Udhhiyah mmoja kwa baba anayeishi na watoto wake watatu


Swali: Baba anaishi pamoja na watoto wake watatu ambao wote wamekwishaoa. Kila mmoja katika wao ana sehemu yake ya kipekee. Je, mnyama mmoja anatosha kwa wote?

Jibu: Vile ninavyoona ni kwamba kila nyumba wanatakiwa kuchinja. Kwa sababu kila nyumba iko kivyake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/38)
  • Imechapishwa: 20/08/2018