Udhhiyah kwa mwenye kuhiji


Swali: Ni jambo limeenea kati ya watu wa kawaida kwamba mwenye kuhiji hatakiwi kuchinja isipokuwa ikiwa kama amekufa mmoja kati ya wazazi wawili. Je, ni sahihi?

Jibu: Si sahihi. Mwenye kuhiji akiwa yeye ndiye baba mwenye nyumba basi anatakiwa kuchinja. Kwa msemo mwingine ni kwamba anatakiwa kuiambia familia yake wachinje Udhhiyah kwa ajili yake yeye na wao na awape kima cha pesa. Lakini kama anakusudia kuchinja Udhhiyah Makkah haifai.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1446
  • Imechapishwa: 09/08/2019