Udhhiyah kwa ambaye ana wake wawili wasioishi nyumba moja

Swali: Kuna mtu ameoa wake wawili ambapo mmoja anaishi naye na mwingine anaishi anaishi kwao na mke. Je, analazimika kuchinja mnyama mmoja au wawili?

Jibu: Achinje katika ile nyumba ambayo yeye anaishi na atamtosha pia huyo mwingine. Kwa sababu mke huyo ni katika familia yake. Ikiwa mwanamke huyo anaishi na familia yake, basi wakati wa kuchinja anuie mnyama huyo ni kwa ajili yake na kwa ajili ya familia yake na hivyo ataingia ndani japokuwa atakuwa anaishi na familia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (25/43)
  • Imechapishwa: 20/08/2018