Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ

“Miongoni mwa watu wako wasemao “Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho hali ya kuwa si wenye kuamini.”[1]

Wanatamka kwa ndimi zao yasiyokuwemo mioyoni mwao. Allaah akawakadhibisha kwa kusema:

وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ

“… hali ya kuwa si wenye kuamini.”[2]

Kwa sababu imani ya kikweli ni ile inayotokana na moyo na mdomo. Shani ya mambo huku ni kumhadaa Allaah na waumini.

Allaah hadhuriki chochote na udanganyifu wao kama ambavo waja Wake waumini hawadhuriki chochote na udanganyifu wao. Waumini hawadhuriki kwa kile kitendo cha wanafiki kuonyesha kuwa wameamini na matokeo yake zikasalimika mali na damu zao na vitimbi vyao vikawarudilia wao wenyewe. Matokeo yake wakapata utwevu na fedheha duniani na huzuni wa kuendelea kutokana ile nguvu na nusura inayowapitikia waumini. Isitoshe Aakhirah watakuwa na adhabu chungu kwelikweli kwa sababu ya uongo, kufuru na uovu wao. Kutokana na ujinga na upumbavu wao hawahisi jambo hilo.

[1] 02:08

[2] 02:08

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 31
  • Imechapishwa: 06/05/2020