Udalali haujumuishwi katika bei ya bidhaa


Swali: Ni ipi hukumu ya kuchukua malipo kwa ajili ya ile kazi na muda wangu wote niliotumia katika kuuza bidhaa?

Jibu: Ni udalali na haina neno.

Swali: Tatizo ni kwamba mteja anafikiria kuwa hiyo ndio bei ya bidhaa.

Jibu: Wabainishie hali halisi ilivyo. Bei ya udalali haikujumuishwa katika bei ya bidhaa. Ima itakuwa kwa yule muuzaji au kwa yule mnunuzi, kutegemea na masharti, lakini hata hivyo haijajumuishwa katika bei ya bidhaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 05/02/2022