Uchafuchafu na umanjano havizingatiwi midhali damu ya hedhi imeshakauka II

Swali: Kuna mwanamke alipata hedhi kisha akajisafisha. Baada ya siku mbili damu ikarudi na ikaendelea kumtoka siku hiyo ambapo hakuswali. Je, kuna kinachomlazimu?

Jibu: Ukitwahirika na ukaona alama za kutwahirika, basi usikae. Damu hii ima ni uchafuchafu au umanjano, vitu ambavyo havizingatiwi. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na uchafu baada ya kutwaharika kuwa ni kitu.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 26/12/2020