Swali: Ni yapi maoni yako kuhusu kusoma kitabu “Manhaj-ul-Muslim” cha Shaykh Abu Bakr al-Jazaairiy?

Jibu: Shaykh Abu Bakr al-Jazaairiy sio marejeleo ya kielimu. Anachanganya vitu na mambo. Ni Tabliyghiy. Mimi nilisoma kwake na hivyo nina ujuzi nae. Anaweza akapatia wakati fulani, lakini vitabu vyake mara nyingi vimejengeka juu ya khitimisho za binafsi. Na asli ni kwamba ni mwandishi wa khabari. Alitoka katika nchi yake akiwa ni mwandishi wa khabari, kama wasemavyo baadhi. Kisha kuna kipindi alisoma katika kitivo cha Shari´ah Riyaadh. Ilikuwa ni kabla ya chuo kikuu cha Imaam [Muhammad bin Su´uwd]. Haistahiki kwamwe kwa mtu kama mfano wake kuwa marejeleo ya kielimu kutokana na makosa yake mengi.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jazaairiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=137163
  • Imechapishwa: 11/01/2018