Uasi kwa kiongozi anayechukua pesa za nchi na anawakandamiza raia


Swali: Je, inajuzu kufanya uasi kwa mtawala na kumwaga damu ili kumuangusha akichukua pesa na kuwakandamiza wananchi?

Jibu: Kuna Hadiyth Swahiyh juu ya hili na kwamba atasikilizwa na kutiiwa maadamu ni muislamu. Hatofanyiwa uasi kwa sababu ya dhuluma yake hata kama atapiga mgongo wako na kuchukua mali yako. Hili bila ya shaka ni madhara, lakini bila ya shaka madhara yatayotokea kwa kumfanyia uasi ni makubwa zaidi. Hili linaingia ndani ya kanuni ya kufanya madhara madogo ili kuepuka madhara makubwa zaidi. Haijuzu kufanya uasi kwa mtawala dhalimu maadamu ni Muislamu. Kutokumfanyia uasi ina maana anatiiwa, watu wanakuwa na umoja, damu inasalimika na kuzuiwa kwa fitina kuwapata waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/7aqoq-01.mp3
  • Imechapishwa: 05/09/2020