Swali: Kuna baadhi wanaita katika uasi na wanasema kwamba uasi uliyokatazwa dhidi ya mkusanyiko wa waislamu ni uasi wa kusimamisha silaha na sio maandamano na mtu kuonesha anayopenda.

Jibu: Kuna aina mbalimbali za uasi. Moja wapo ni kwa maneno. Ikiwa anaita watu katika uasi na akawavutia katika uasi dhidi ya mtawala, huu ni uasi. Huu ni uasi hata kama hakunyanyua silaha. Pengine hili likawa khatari zaidi kuliko kunyanyua silaha. Yule mwenye kueneza madhehebu ya Khawaarij na akavutia katika uasi, huyu ni khatari zaidi kuliko kunyanyua silaha. Uasi unaweze vilevile kuwa kwa moyo pale ambapo ataonelea kuwa mtawala hastahiki kuwa mtawala na yaliyo ya wajibu kwake na akawachukia watawala wa Waislamu. Huu ni uasi kwa moyo.

Uasi unaweza kuwa kuwa kwa moyo, nia, maneno na silaha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14279
  • Imechapishwa: 05/09/2020