Uashiriaji wakati wa kutaja sifa sio kufananisha

Swali: Tumekuona ukiashiria kwa kidole chako ulipokuwa unasema Hadiyth ya kuwa Allaah ataweka mlima kwenye kidole Chake. Je, hili linajuzu?

Jibu: Ndio, kwa njia ya kuhakikisha sifa. Kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Allaah alimuumba Aadam hali ya kuwa ni mwenye kusikia na mwenye kuona.”

Halafu akaashiria kwenye masikio yake na macho yake. Hili ni kwa njia ya kuhakikisha sifa. Hakukusudiwi kufananisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/AbdelazizRajhi/Tahauiya2/02.mp3
  • Imechapishwa: 06/09/2020