Uadilifu ni kumpa kila mtoto mmoja kile anachohitajia

Swali: Kuhusu maudhui ya kufanya uadilifu kati ya watoto. Ikiwa mmoja katika watoto anafanya kazi na baba yake kwenye kilimo na ndugu wengine wamesoma, je, inafaa kwa baba kumsaidia mtoto wake huyu juu ya kuoa kwake katika kuzalisha ardhi kutokamana na wale wanyamaza alionao?

Jibu: Ikiwa mtu yuko na watoto ambapo baadhi yao wanajitosheleza kwa njia ya kwamba wana mishahara, biashara na mwengine akawa hana kitu ambapo akahitajia kuoa, basi ni wajibu kwa baba kumuoza. Asiwape wale wengine sawa na kiwango kilekile. Isipokuwa ikiwa kama na wao watahitajia kuoa na wakawa hawana kitu, basi awaoze kama alivyomuozesha huyu. Nataka kuwapa kanuni: mambo yanayohusiana na matumizi, uadilifu ni kumpa kila mmoja anachohitajia. Kuoa kunaingia katika matumizi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/815
  • Imechapishwa: 23/02/2018