Twawaaf-ul-Ifaadhwah Miaka Mitatu Baada Ya Hajj

Swali: Miaka mitatu ya nyuma nilihiji bila ya kufanya Twawaaf-ul-Ifaadhwah. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Nenda na ufanye Twawaaf-ul-Ifaadhwah. Wakati haujatoka. Ikiwa ulifanya jimaa katika wakati huo unatakiwa kutoa fidia ya kuchinja kondoo Makkah na kuigawa kwa mafukara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14331228.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015