Twawaaf na Sa´y na manukato wakati wa Ihraam

Swali: Kuna mtu amefanya Twawaaf na Sa´y na mabaki ya manukato katika Ihraam yake ambayo hakuiosha. Je, kitendo chake ni sahihi au ni lazima atoe fidia?

Jibu: Kama alikuwa hajui kuhusu hilo, hakuna kinachomlazimu. Lakini kama alifanya hivo kwa kukusudia ni lazima atoe fidia. Ima achinje kondoo, awalishe masikini sita au afunge siku tatu. Ninachomaanisha ikiwa alijui kuhusu manukato hayo na wala hakuiosha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (21) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 14/02/2020