Twawaaf na kukhitimisha Qur-aan kwa ajili ya maiti

Swali: Inatokea wakati mwingine kumfanyia Twawaaf mmoja katika ndugu zangu, wazazi wangu au mababu na mabibi waliofariki. Nini hukumu ya hilo? Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan nzima kwa ajili yao?

Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo. Kwani hakuna dalili ya hayo. Lakini imependekezwa kuwatolea swadaqah wale utakaowataka katika jamaa zako na wengineo muda wa kuwa ni waislamu, kuwaombea du´aa, kuwafanyia hajj na ´umrah.

Kuhusu kuswali, kufanya Twawaaf na kusoma Qur-aan kwa ajili yao bora ni kutokufanya hivo. Hakuna dalili ya hayo. Wako wanazuoni walioyajuzisha hayo kwa kutumia kipimo cha swadaqah na du´aa. Lakini lililo salama zaidi ni kutokufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/344)
  • Imechapishwa: 18/06/2021