Twawaaf juu ya kiti cha magurudumu au gari

Swali: Je, inafaa kwa ambaye ni muweza kufanya Twawaaf kwenye kiti cha magurudumu?

Jibu: Hakuna neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya Twawaaf hali kukaa juu ya mnyama. Wakati watu waliposongamana kwake, aliketi juu ya mnyama. Alifanya hivo ili watu waweze kumuona na aepuke msongamano. Inafaa kufanya Twawaaf hali ya kukaa, kufanya Sa´y´ hali ya kukaa, juu ya mgongo wa ngami au gari. Hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/04/2020