Twahara ya kupangusa juu ya soski inaondoka kwa kule kuzivua?


Swali: Kuna mtu amepangusa juu ya soksi wakati alipokuwa anatawadha kisha akazivua baada ya kuwa na harufu mbaya ambapo akaswali na hakuosha maeneo pale [pa mguu]. Ni ipi hukumu ya swalah yake akiwa katika hali hii?

Jibu: Ikiwa amezivua akiwa katika twahara yake ya kwanza ambayo alivaa juu yake soksi, basi twahara yake ni yenye kubaki. Hakumdhuru kitu kuivua kwake. Lakini ikiwa kuzivua kwake soksi ilikuwa baada ya kupatwa na hadathi, basi wudhuu´ wake unachenguka. Hivyo atalazimika kurudia kutawadha. Kwa sababu hukumu ya twahara ya kupangusa juu ya soksi imeondoka kwa kule kuzivua kwake soksi kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/113)
  • Imechapishwa: 15/08/2021