Twaaghuut kwa anayehukumu kinyume na Shari´ah

Swali: Mwenye kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah anaitwa kuwa ni Twaaghuut?

Jibu: Ndio, anaitwa kuwa ni Twaaghuut japokuwa hatohalalisha. Kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah na Twaaghuut vimegawanyika aina kubwa na ndogo.

Swali: Mwenye kusema kuwa kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah kunatofautiana na uzinzi na hukumu zengine?

Jibu: Mimi sijui. Ni kama walivoweka wazi Maswahabah kama ´Abdullaah bin ´Abbaas na wengineo kwamba ni kufuru ndogo. Je, mtu akimuhukumia kwa kupendelea ndugu yake, baba yake, mama yake, rafiki yake au mali yake juu ya hukumu fulani ilihali anajua kuwa amekwenda kinyume na haki anakufuru?

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 14/07/2019