Swali: Je, una nasaha zozote kuwapa wale wanaotazama dishi mchana au usiku wa Ramadhaan?

Jibu: Nasaha zangu ni kuhusu wale wanaotazama Ramadhaan na katika miezi mingine. Nyinyi mnajua kumepitika nini kupitia dishi hizi jinsi jamii zimebadilika na khaswa vijana. Kuna mabadiliko ya wazi. Tangu kujitokeze kifaa hiki chenye kuharibu na sisi wenyewe tunahisi mabadiliko. Madhara yake ni makubwa. Tunamuomba Allaah aifanye serikali kuwashughulikia wale wanaozitumia ili waweze kuzivunja. Kwa sababu ukweli wa mambo ni kwamba zina madhara. Ni mamoja upande wa dini, tabia, amani na kwa njia zengine zote. Yule ambaye yuko nayo hakuna njia nyingine ya kujikwamua nayo isipokuwa kwa kuivunja. Kwa sababu akiipeana zawadi huyo mwingine ataitumia katika maasi na yeye aliyetoa zawadi atakuwa ndiye sababu. Vivyo hivyo akiiuza. Kwa hivyo hakuna njia ya kujinasua nayo isipokuwa kwa kuivunja. Akiuliza ni vipi ataivunja ilihali yeye ameinunua kwa pesa na kwamba huku ni kuharibu pesa? Tunamjibu kwa kumwambia kuharibu pesa katika kumtii Allaah ni jambo la kheri. Pesa zote Allaah anampa nazo mtu ili zimsaidie kumtii Yeye. Kwa hivyo tukiziharibu kwa kuchelea tusije kutumbukia ndani ya maasi, basi huko inakuwa ni kushinda na kufaidika na sio kuharibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1391
  • Imechapishwa: 07/12/2019