TV ni shaytwaan katika nyumba ya muislamu

Huyu – yaani TV – ni Shaytwaan aliyefukuzwa mbali na rehema za Allaah katika nyumba ya muislamu…

TV madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake. Maneno yako kwamba ndani ya TV kuna faida vilevile. Haistahiki wakati mwingine – na wewe ni muislamu – haitakiwi kusema maneno kama haya. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu pombe:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا

”Wanakuuliza kuhusu pombe na kamari. Sema: “Katika viwili hivyo mna dhambi kubwa na manufaa [fulani] kwa watu; na dhambi yake viwili hivyo ni kubwa kuliko manufaa yake.”[1]

Haijuzu kwa mtu kukitazama kitu upande mmoja kwamba kina manufaa lakini akasahau madhara. Ikiwa kitu kina manufaa na madhara basi anatakiwa kupima; ikiwa madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake basi kitakuwa ni haramu. Ikiwa manufaa yake ni makubwa zaidi kuliko madhara yake basi kitakuwa ni halali.

TV, ijapokuwa kuna faida inayotambulika na kila mtu, lakini hata hivyo shari yake ni kubwa kuliko faida yake. Kwa mfano nitawauliza swali moja tu; mnaweza mkanambia kuna nyumba yoyote ambayo ndani kuna TV na watu  wa nyumba hiyo wanalala punde tu baada ya swalah ya ´Ishaa au hukesha mpaka katika nusu ya usiku? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kulala kabla ya swalah ya ´Ishaa na kukesha baada yake…

Kwa hivyo basi mche Allaah juu ya nafsi yako na kwa wale uliochungishwa.

[1] 02:219

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=TQTiKdRG5z0
  • Imechapishwa: 29/04/2018