Tusinunue bidhaa za makafiri kwa sababu tunawatia nguvu?

Swali: Inajuzu kununua kutoka kwa makafiri? Wapo wanaosema kwamba kufanya hivo kunawapa nguvu makafiri upande wa uchumi na kwamba huku ni kuwasaidia dhidi ya waislamu.

Jibu: Haya ni maneno ya mjinga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alinunua kutoka kwa makafiri na mayahudi na akafanya nao biashara. Waislamu wanafanya biashara na makafiri. Haya yana manufaa kwa waislamu. Sio kuwapa nguvu makafiri. Ni wapi utanunua magari na nguo. Bidhaa zote za duniani hii leo zinafanywa na wao. Hivyo usinunue kutoka kwao chochote. Tembeeni pasi na nguo na mtembee pasi na vipando na mseme kuwa eti ni kuwasusa makafiri. Haijuzu kusema hivi. Madhara bado yatawarudilia waislamu. Waislamu wanafurahishwa na hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidhl-il-Islaam (08) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/08.mp3
  • Imechapishwa: 15/02/2019