Hii leo kuna mifano mingi katika watu mnaowajua waliokuwa wakifuata mfumo wa Salaf. Pindi walipoanza kuchanganyikana na Ahl-ul-Bid´ah wakapotea. Kwa sababu Ahl-ul-Bid´ah hii leo wana mbinu nyingi, nishati kwelikweli na mifumo – kuna uwezekano ndio mifumo iliyokuwa ikitambuliwa na mashaytwaan hapo kitambo – na wao hivi sasa wakazijua mbinu hizi, mifumo hii na namna watakavyowadanganya watu.

Miongoni mwa mbinu za Ahl-ul-Ahwaa´ wa hivi sasa ni pamoja na kwamba unatakiwa kusoma kila kitu na uchukue haki na uache yale ambayo ni batili. Vijana wengi hawajui haki kutokamana na batili na wala hawawezi kupambanua haki kutokamana na batili. Matokeo yake wanatumbukia katika batili huku wakiona kuwa ni haki na wanaitupilia mbali haki wakiona kuwa ni batili. Mambo yamewapindukia. Kama alivyosema Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh):

“Hakika upeo wa upotevu ni wewe kupinga yale [siku moja] ulokuwa ukiyatambua na kuyatambua yale [siku moja] ulikuwa ukiyapinga.”

Utayaona haya ni yenye kupitika katika safu ya Salafiyyuun isipokuwa wale waliosalimishwa na Allaah. Ghafla utaona masikini huyu kishategwa. Tahamaki utaona anawapiga vita Ahl-us-Sunnah, maovu kwake yamekuwa ni mema, mema kwake yamekuwa ni maovu. Huu ndio upeo wa upotevu kabisa.

Kwa hivyo sisi tunawatahadharisha vijana Salafiyyuun kudanganyika na Ahl-ul-Bid´ah na kulemea kwao.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=325§
  • Imechapishwa: 11/06/2017