Tunamsalimia mzushi?


Je, tumsalimie mtu wa Bid´ah? Jawabu linahitajia upambanuzi.

Ikiwa Bid´ah ni za ukafiri, basi hatumsalimii. Kwa sababu haijuzu kumsalimia kafiri.

Ikiwa Bid´ah hizo hazifikii kiwango cha ukafiri, kama mfano wa baadhi ya fikira ambazo hazimtoi mtu nje ya dini na mfano wake, basi mtu atatazama kama kule kuacha kumsalimia kuna manufaa basi inapasa kuacha kumsalimia. Ni vipi kunaweza kuwa kuna manufaa katika kuacha kumsalimia? Ndio, ni pale atapotambua kuwa amekatwa kwa sababu ni mzushi. Matokeo yake akaacha Bid´ah yake na kutubu. Hivyo italazimika kumsusa kwa sababu kunamfanya kutubia.

Ikiwa ukataji haumzidishii kitu isipokuwa tu madhara na kuzidi kufanyia kazi Bid´ah na kulingania kwayo, basi hatumsusi kwa vile ni muislamu. Haijuzu kumkata muislamu.

  • Mhusika: Imâm Muhammad bin Sâlih bin ´Uthaymîn (d. 1421)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (13)
  • Imechapishwa: 10/07/2021