Tunamhukumu mtu kwa matamshi yake ya talaka na si kwa nia

Swali: Mtu akitamka Talaka, ni ipi hukumu ikiwa kwa Talaka hiyo ananuia yamini?

Jibu: Akitamka Talaka, tunamhukumu kwa matamshi yake na wala hatutazami nia yake. Tunamhukumu matamshi yake ya Talaka ya wazi aliotamka. Na wala hatujali kwa ubabaishaji wa kusema: “Mimi sikukusudia, mimi hivi na vile”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/10050
  • Imechapishwa: 07/02/2018