Tunalingania kwa Allaah na tunapuuzilia mbali tuhuma za watu hawa

Swali: Ni vipi tutawaraddi wale wanaosema kwamba wanachuoni hawakatazi maovu na wanaeneza hayo baina ya watoto wa jamii.

 Jibu: Huyu hayo ambayo anakusudia huenda si maovu kamwe ni mambo anayofikiria na si maovu ya kweli. Huyu huenda anataka kukemea haki. Kwa kuwa wapo watu ambao wanazingatia haki kuwa ni maovu, wanazingatia kwamba kulingania kwa Allaah ni maovu na kujiingiza katika mambo ya watu na kadhalika. Akilini mwao haki imegeuka kuwa batili, wanaona ni kuingilia mambo ya watu, ni kuwa na dhana mbaya kwa watu na tuhuma nyenginezo. Tunapuuzia mbali wasiwasi huu. Tunafikisha kheri, tunalingania kwa Allaah na tunawafunza watu kheri. Ambaye anataka kutukosesha nusura hatotuathiri kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17749
  • Imechapishwa: 04/04/2018