Tuko katika zama za Jaahiliyyah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kuwa wakati huu ni wa Jaahiliyyah yenye kuenea?

Jibu: Ni mwongo. Baada ya kutumwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imeondoka Jaahiliyyah yenye kuenea. Himdi zote ni za Allaah Uislamu upo, Qur-aan na Sunnah vipo. Hatuko katika Jaahiliyyah yenye kuenea. Ingawa kunaweza kuwepo Jaahiliyyah katika baadhi ya watu na baadhi ya makabila.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17492
  • Imechapishwa: 21/11/2017