Ahmad al-Ghumaariy amesema:

“Tambua kwamba Hadiyth zilizopokelewa juu ya watokaji ni zenye kufanana na Hadiyth za Khawaarij. Hata kama wote ni wenye kutoka katika dini (خوارج عن الدين) na wote ni mijibwa ya Motoni, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pamoja na hivo wamegawanyika mafungu mawili:

1 – Fungu la kwanza wanatambulika kwa jina hili. Wamesifiwa kuwa ni wenye kujikakama na kuchupa mpaka katika dini na kwamba mmoja wetu atazidharau swalah na swawm zake ukilinganisha na swalah na swawm zao.

2 – Fungu la pili ni wale wapotofu wa sasa (ملاحدة العصر). Wamesifiwa kuwa wapumbavu na vijana na kwamba alama zao ni kunyoa upara.

Pindi kulipozuka pembe ya shaytwaan huko Najd mwishoni mwa karne ya kumi na fitina yake ikaenea, basi wanachuoni wote walikuwa wakizitumia Hadiyth hizi juu yake na wafuasi wake, kwa sababu kulikuwa hakujazuka aina ya Khawaarij hawa hapo kabla.”[1]

Tatu: Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ

“Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi hakikisheni msije mkawasibu watu kwa ujinga, mkaja kuwa wenye kujuta juu ya ambayo mmeyafanya.” (49:06)

Katika utangulizi mtunzi wa kitabu ametaja kwamba yeye ni miongoni mwa wale wanaofuata Qur-aan na Sunnah halafu baadaye maneno yake yakaenda kinyume na kitendo chake katika maeneo mengi ndani ya kitabu chake. Maudhui haya ni miongoni mwa maeneo hayo. Kwa sababu hakuhakikisha juu ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na watu wa Najd. Badala yake amekurupuka kuwatuhumu kwa kitu ambacho ukweli wa mambo hakiendani nao. Lau angelithibitisha kama wanavofanya wanachuoni wengine juu ya jambo la Shaykh na watu wa Najd, basi ingelimbainikia kuwa Shaykh na watu wa Najd hawana lolote kuhusiana na yale ambayo wapindaji na wapotofu wanamtuhumu kwayo.

[1] Mutwaabaqat-ul-Ikhtara´aat al-´Aswriyyah, uk. 76

  • Mhusika: ´Allaamah Hamuud bin ´Abdillaah at-Tuwayjiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iydhwaah-ul-Mahajjah, uk. 139
  • Imechapishwa: 07/07/2020