Miongoni mwa uzushi wa Dahlaan ni kwamba anasema kuwa eti Ibn ´Abdil-Wahhaab alikuwa akidhamiria akitaka kudai utume. Lakini alipoona kuwa watu hawatomsadikisha ndio akanyamazia fikira hii. Vinginevyo ni kitu kilikuwa moyoni mwake[1]. Ni kama kwamba Dahlaan huyu anajua yaliyomo ndani ya moyo na anajua mambo yaliyofichikana. Kuna uongo na uzushi mwingine wa kuchekesha.

Kwa hiyo Shaykh si yeye peke yake ambaye alituhumiwa na akawekewa shubuha katika Da´wah yake. Ikiwa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) walituhumiwa basi wafuasi wao wana haki zaidi ya kufanyiwa hivo. Amesema (Ta´ala) kumwambia Mtume Wake:

مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ

“Hakusemwi juu yako isipokuwa kile walichoambiwa Mitume kabla yako. Hakika Mola wako ni Mwenye msamaha na Mwenye adhabu iumizayo.”[2]

[1] Tazama “Swiyaanat-ul-Insaan ´an Waswasat-ish-Shaykh Dahlaan”, uk. 512.

[2] 41:43

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydatu al-Imaam-il-Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 143-144
  • Imechapishwa: 24/01/2020