Tofauti ya waumini na makafiri wakati wa mitihani na majanga

Wakati wa ukame ni lazima kumwomba Allaah kuteremsha mvua. Wakati kunapoteremka magonjwa na maradhi ya mlipuko ni lazima kumwomba Allaah usalama. Allaah anajaribu na kutahini kwa majanga na kwa neema. Hivi sasa tunasikia wanaopinga du´aa na mfano wa hayo na wanadai kuwa mambo kama hayo ni ya kawaida na kwamba yataondoka:

قَدْ مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

”Hakika iliwagusa baba zetu madhara na raha. Basi tukawachukuwa [kwa kuwaadhibu] ghafla nao huku hawahisi.”[1]

Nyoyo zao hazilainiki, bali uovu wao ndio unaongezeka. Wanapinga du´aa, swalah ya kuomba mvua na mfano wa hayo. Wanasema kuwa kilichoteremka sio adhabu na kwamba ni kitu cha kilimwengu kilichowapitikia hata wale waliokuwa kabla yetu na baadaye kikaondoka na kwamba na sisi kitatuondokea. Hivo ndivo wanavofikiria. Wanaona kuwa ni majanga ya kikawaida yaliyofungamana na mazingira.

[1] 07:95

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://mobile.twitter.com/thealtawhid/status/1242307296149061632
  • Imechapishwa: 23/04/2020