Tofauti ya wanachuoni juu ya tawbah ya mchawi, mwenye kumtusi na kumfanyia mzaha Allaah na Mtume

Swali: Mchawi anatakiwa kuambiwa atubie au anatakiwa kuuawa pasi na kutakwa kutubia?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana juu ya mchawi. Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa hatakiwi kuambiwa atubie. Hukumu yake ni kama zandiki, mnafiki, mwenye kumtusi Allaah, Mtume, mwenye kufanya mzaha na Allaah, Mtume wake, Qur-aan na dini Yake.

Mchawi, zandiki, mwenye kumtusi na kumfanyia mzaha Mtume linalotambulika kwa wale wahakiki wote ni kwamba hatakiwi kuambiwa kutubia. Kwa sababu tawbah yake haikubaliwi katika mambo ya kidunia. Ni lazima asimamishiwe adhabu ya Kishari´ah japokuwa atadai kuwa ametubia. Hilo linawaogofya watu kutokamana na kufuru hii kubwa. Kuhusu huko Aakhirah tawbah yake ni yenye kukubaliwa ikiwa ni mkweli. Allaah (Ta´ala) ataikubali tawbah yake.

Wanachuoni wengine wakasema inapaswa kumtaka atubie hata kama atakuwa ni mwenye kutusi, kufanya maskhara na mchawi. Akitubia ni sawa. Vinginevyo anauawa. Hata hivyo hili linarudi kwa yule hakimu wa Kishari´ah. Ana haki ya kuchagua moja ya maoni haya mawili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 03/01/2018