Tofauti ya ukale na uzukaji kati ya Ahl-us-Sunnah na Ibaadhiyyah inapokuja katika maneno ya Allaah


Maana ya ukale na kuzuka, maana yake kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah ni yale niliyoyataja, kwamba sifa ya maneno Allaah (Ta´ala) anasifika nayo kwenye dhati Yake na kwamba anatamka kwa kutaka na kwa khiyari Yake pindi anapotaka na kwa namna anayoitaka:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

Ama kwa mujibu wa al-Khaliyliy na wahenga wake Mu´tazilah, wao wanapinga sifa ya maneno anayosifika nayo Allaah (Ta´ala) na wanaabiria juu ya kuumbwa kwa Qur-aan kwa tamko “kuzuka”. Anachokusudiwa kwa “kuzuka” ni kuumbwa. Hayo ameyaweka wazi.

[1] 42:11

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 242
  • Imechapishwa: 15/04/2017