Tofauti ya swalah hizi mbili

Mtu hawezi kulinganisha kitendo cha kuswali katika msikiti ulio na kaburi na kuswali katika ardhi ilioporwa au nguo ilioporwa. Kwa sababu kwanza kuswali katika ardhi ilioporwa na nguo ilioporwa ni jambo wanachuoni wametofautiana. Hanaabilah na kundi la wanachuoni wengine wanaona kuwa kuswali katika ardhi ilioporwa na nguo iliopotwa swalah haisihi. Kujengea juu ya maoni ambayo yanasema kuwa swalah inasihi – na ndio maoni sahihi – hakulinganishwi kati ya hayo mawili. Kwa sababu kitendo hichi kimekataliwa kama kilivyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiyafanye makaburi kuwa ni sehemu ya kuswalia.”

Kuswali katika ardhi ilioporwa ni jambo limekatazwa. Ni mamoja mtu ameswali sehemu hiyo au hakuswali. Ama kuhusu kuswali katika msikiti ambao uko na kaburi ni jambo limekatazwa kama lilivyo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah awalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu ya kuswalia. Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa ni sehemu ya kuswalia.”

Ni jambo limekatazwa kama lilivyo. Kwa sababu ni miongoni mwa mambo yanayopelekea katika shirki. Swalah haiwezi kukubalika Kishari´ah mahali ambapo ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 09/11/2018