Tofauti ya pombe ya duniani na Aakhirah

Swali: Sote tunajua uharamu wa pombe duniani, kwamba inalevya na kwamba inaondosha akili. Kwa ajili hii ni chukizo kutokana na kitendo cha shaytwaan na kwamba ndiye mama wa machafu, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Swali langu Shaykh: ni kwa nini pombe duniani imeharamishwa lakini Aakhirah ikahalalishwa?

Jibu: Pombe ya Aakhirah ni nzuri; haina ulevi, madhara wala chenye kuudhi. Kuhusu pombe ya duniani inayo madhara, ulevi na mambo yenye kuudhi. Hiyo ina maana kwamba pombe ya Aakhirah haiondoshi akili, fahamu wala ndani yake hamna kitu kinachodhuru mwili. Kuhusu pombe ya duniani inadhuru akili na mwili vyote viwili. Madhara yote yanayopatikana katika pombe ya duniani hayapatikani katika pombe ya Aakhirah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/492)
  • Imechapishwa: 15/12/2020