Swali: Ni ipi hukumu ya kushiriki katika mashindano mbalimbali ikiwa kuna tuzo kama gari na pesa?

Jibu: Kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia. Ikiwa mashindano yanahusiana na mpira wa miguu au kitu kingine kinachokushughulisha, basi nakunasihi kujitenga nacho mbali. Hawakuviweka isipokuwa tu ni kwa sababu wanataka kukushughulisha kutokamana na elimu yenye manufaa.

Kuhusu mashindano ya Qur-aan au kuhifadhi Hadiyth au mambo ya ki-Fiqh au maswali ya kisarufi, hilo litarudi katika nia yako. Ukiona kuwa nia yako ni kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) peke yake, basi fanya mashindano. Ama ukiona nia yako kwa ajili ya kitu kingine kama mali, nakunasihi ujiepushe.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=4395
  • Imechapishwa: 19/02/2017