Tofauti ya maombi ya Muusa na mayahudi kumuona Mola wao


Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ

“Alipokuja Muusa katika miadi Yetu na Mola wake akamsemesha, [Muusa] alisema: “Mola wangu! Nionyeshe ili nikutazame.” Akasema: “Hutoniona, lakini tazama mlima ukitulia mahali pake basi utaniona.” Mola wako alipojidhihirisha kwenye mlima akalifanya lisambuke kuwa vumbi na Muusa akaanguka hali ya kuzimia. Alipozindukana akasema: “Utakasifu ni Wako! Nimetubu Kwako nami ni wa kwanza wa wanaoamini.” (07:143)

Ni wapi katika Aayah hii ambapo wana wa israaiyl walimuomba Muusa awaonyeshe Allaah waziwazi kama ambavyo hayo yalivyothibiti katika Aayah nyingine[1] ambapo Allaah amebainisha msimamo huo waliochukua wana wa israaiyl pamoja na Mtume wao (´alayhis-Salaam) kwa kuuliza maswali ya kupindukia na kuwa na utovu wa adabu na Mtume wa Allaah Muusa na nduguye Haaruun (´alayhimaas-Salaam) mpaka wakaenda kumuabudu ndama. Hakika, wewe al-Khaliyliy, hukukusudia kutaja Aayah isipokuwa ilikuwa kutaka kuwapaka watu mchanga wa machoni. Vinginevyo ni kwamba wewe unaelewa kupitia maneno ya wafasiri wa Qur-aan ya kwamba kilichokusudiwa katika Aayah ile ilikuwa ni makatazo ya kuvuka mipaka ambayo mayahudi walikuwa wakimuuliza nayo Muusa (´alayhis-Salaam). Bila shaka unayajua hayo lakini matamanio na kupenda kupotosha kunamzuia mwenye nayo kutokamana na njia iliyonyooka.

[1] 02:55

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 70
  • Imechapishwa: 14/01/2017