Swali: Kuna vidhibiti vipi katika kuwakufurisha watu kwa dhati zao? Kwa sababu wapo wanachuoni wanasema kwamba asikufurishwe yeyote kwa dhati yake, hata akiwa ni myahudi, mpaka kuthibiti kwetu chenye kumkufurisha?

Jibu: Mwenye kudhihirisha ukafiri basi anahukumiwa ukafiri. Mwenye kumshirikisha Allaah anahukumiwa kwamba ni mshirikina. Lakini usimkatie Moto. Wewe unamhukumu ukafiri hapa duniani kwa mujibu wa yale anayofanya. Kuhusu Aakhirah usimhukumu kwamba ataingia Motoni. Kwa sababu huenda alitubia pasi na wewe kujua. Muulizaji amechanganya kati ya hayo mawili; amechanganya masuala ya kukufurisha na kumhukumu mtu kwa dhati yake kwamba ni wa Motoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 96
  • Imechapishwa: 29/09/2018