al-Khaliyliy, kwenye ukurasa wa 125, anadai kuwa Ibaadhiyyah wanaafikiana na al-Hanaabilah. Hapa tunakuorodheshea maneno yake kwanza halafu baadaye tutayajadili. al-Khaliyliy amesema:

“Kuhusu sisi Ibaadhiyyah ambao tunaonelea kuwa Qur-aan imeumbwa na wale wenye kuonelea kama tunavyoonelea katika Mu´tazilah na wengineo. Tumeafikiana vilevile na Hanaabilah wenye kuonelea kuwa maandiko ya Qur-aan ni ya tangu hapo kale juu ya kwamba Muusa (´alayhis-Salaam) aliyasikia maneno ya Allaah alipozungumza yaliyo na herufi na kwamba ilikwa ni sauti. Isipokuwa tu tumetofautiana juu ya ukale wake na kule kuzuka/kuumbwa kwake. Wao wanaonelea kuwa ni ya tangu hapo kale/milele na sisi tunaonelea kuwa ni yenye kuzuka/kuumbwa. Sisi tumesema kuwa kule Allaah kumzungumzisha ni jambo la kikweli. Kwani hapakuwa kizuizi. Uhakika wa mambo ni kuwa Allaah alimuumbia nayo pale anapopataka akamsikizisha nayo pasi na kumtamkisha nayo Malaika au kiumbe mwengine.”

Huu ni uongo. Hanaabilah hawaonelei kuwa Allaah kumzungumzisha Muusa ni jambo la kale. Bali ni jambo lilitokea katika wakati wake[1]. Ubainifu wa hayo utakuja huko mbele tukijibu madai haya.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/msimamo-wa-ahl-us-sunnah-juu-ya-maneno-ya-allaah-azza-wa-jall/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 241
  • Imechapishwa: 15/04/2017