´Aqiydah ilio salama inasalimisha damu na mali ya mtu na inafanya vilevile matendo yote ya mtu kuwa sahihi. ´Aqiydah ilioharibika inaangamiza damu na mali ya mtu na inafanya vilevile matendo yote kuharibika. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Kwa hakika umeletewa Wahy na kwa wale walio kabla yako [kwamba]: “Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako, na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” (39:65)

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Na kama wangemshirikisha bila shaka yangeliporomoka yale yote waliyokuwa wakiyatenda.” (06:88)

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kubadili Dini yake muueni.”

“Damu ya mtu muislamu sio halali isipokuwa kwa moja ya mambo matatu; mzinifu ambaye kishaoa au kuolewa, mtu kumuua mwingine na mwenye kuacha dini yake mfarikishaji wa mkusanyiko.”

Hii ni dalili inayoonyesha kuwa kuwa na ´Aqiydah ilio salama inamlindia mtu damu na mali yake. Damu na mali yake sio halali midhani ´Aqiydah yake ni sahihi isipokuwa pale atapofanya moja kati ya hayo matatu: kuzini baada ya kuingia katika ndoa, mwenye kuua kwa kukusudia na mwenye kuritadi ambaye amefarikiana na dini yake.

´Aqiydah ikiwa sahihi basi inasahihisha matendo mengine yote. Ikiwa ´Aqiydah ni sahihi basi swalah, swawm, hajj na matendo mengine yote yanakuwa sahihi. Upande mwingine ´Aqiydah ikiharibika matendo mengine yote pia yanaharibika. Mtu akimuomba mwingine asiyekuwa Allaah, akamchinjia mwingine asiyekuwa Allaah, akaweka nadhiri kwa mwingine asiyekuwa Allaah, akatufu kwengine kusipokuwa kwenye Nyumba ya Allah au akafanya jambo lingine miongoni mwa mambo yanayovunja Uislamu, au mtu akaamini kuwa Swalah, Zakaah au Hajja sio wajibu, au akaamini kuwa uzinzi, pombe, ribaa au kuwaasi wazazi wawili ni halali, ´Aqiydah yake inaharibika na matendo yake mengine yote pia yanaharibika. Swalah yake, Zakaah, Swawm, Hajj wala matendo mengine yote hayatosihi na yanakuwa ni batili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (22-23/01)
  • Imechapishwa: 07/06/2020