Amesema (Ta´ala):

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا

“Sema: “Ikiwa watakusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan, basi hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.”[1]

Ni vipi kiumbe aliyeumbwa kwa udongo maneno yake yanaweza kuwa kama maneno ya Mola wa viumbe? Vipi mpungufu na ambaye ni fakiri kwa kila njia anaweza kuleta maneno kama mfano wa maneno ya mkamilifu ambaye anao ukamilifu usiyofungamana na kujitosheleza kwa kila njia? Haya hayamo ndani ya imkani wala uwezo wao.

Kila ambaye ana ubingwa na maarifa ya maneno mbalimbali akiilinganisha Qur-aan hii tukufu na maneno mengine ya waandishi basi atajiona mwenyewe tofauti kubwa.

[1] 17:88

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 35
  • Imechapishwa: 12/05/2020