Tofauti kati ya tawbah ya moyo na tawbah ya mdomo tu

Swali: Kuna mtu ametenda dhambi kisha anatubu. Lakini anafanya dhambi mara nyingine. Atajikwamua vipi?

Jibu: Kuwa mkweli pamoja na Allaah. Kwa sababu miongoni mwa sharti za tawbah ni kuazimia kutorudi kwenye dhambi hiyo. Ama tawbah yako hii ni tawbah ya waongo na sio tawbah ya wakweli. Kuna tofauti kati ya kutubu kwa mdomo na kutubu kwa moyo. Wewe umetubu kwa mdomo wako lakini hukutubu kwa moyo wako. Dalil ya hilo ni kuwa tawbah haikukuathiri kabisa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Swifaat-il-Mu´miniyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-09/s_0.mp3
  • Imechapishwa: 22/09/2022