Tofauti kati ya mkweli na mzembe

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Maswahabah wengi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) waliota kwamba usiku wa Qadr unatokea tarehe ishirini na saba. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Naona kuwa ndoto zenu zimeafikiana katika zile nyusiku saba za mwisho. Kwa hiyo yule mwenye kuutafuta basi azitafute katika zile nyusiku saba za mwisho.”[1]

Bi maana katika mwaka huo. Vinginevyo miaka mingine unakuwa katika zile nyusiku kumi za mwisho. Kwa msemo mwingine sio usiku maalum. Hata hivyo usiku wenye matarajio makubwa ni wa tarehe ishirini na saba. Kwa mfano mwaka huu unaweza kutokea tarehe ishirini na saba. Mwaka wa pili ukatokea usiku wa tarehe ishirini na moja. Mwaka wa tatu ukatokea usiku wa tarehe ishirini na tano na kadhalika. Allaah (´Azza wa Jall) amefanya kutofahamika kwa faida mbili kuu:

1-Abainike mkweli katika kuutafuta kutokamana na mvivu. Kwa sababu mtu ambaye ni mkweli hajali kujichosha nyusiku kumi kwa ajili ya kuupata usiku wa Qadr. Hata hivyo mvivu ataona uvivu kusimama kuswali nyusiku kumi kwa ajili ya usiku mmoja.

2- Kiasi ambavo muislamu atafanya matendo kwa wingi ndivo atavyolipwa kwa wingi. Kwa sababu kila ambavo matendo yanavokuwa mengi ndivo thawabu pia zinakuwa nyingi.

[1] al-Bukhaariy (2015) na Muslim (1165).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr al-Qur-aan al-Kariym, Juz’ ´Amma, uk. 277
  • Imechapishwa: 15/05/2020