Tofauti kati ya Maswahabah na Jamaa´at-ut-Tabliygh


Ukiwauliza – Jamaa´at-ut-Tabliygh – ni vipi mnatoka makumi [kwa ajili ya kulingania], wanasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akituma makumi ya Maswahabah kuwalingania na kuwafunza watu. Alimtuma Mu´aadh peke yake. Akamtuma Abu Muusa peke yake. Alimtuma Abu ´Ubaydah al-Jarraah kwenda Bahrain peke yake na kadhalika. Kwa sababu walikuwa wanazuoni. Lakini faida iko wapi pinti mnapotuma kikosi cha watu wajinga? Wanatumia hoja kwa mambo ambayo yako dhidi yao.

Mimi nawaambia waketi chini misikitini na wasome. Wakati mmoja wenu atakapojifunza kiasi cha kutosha kitamchomfanye yeye kuhisi kuwa anastahiki, basi atafanya na kusafiri huku na kule na kuzungumza ndani ya misikiti na jamii. Lakini hawafanyi hivo. Ni kwa nini? Ndio, kwa sababu shaytwaan ameketi kwenye njia ya mtu na anamfanyia ugumu njia ya kuiendea kheri na anamfanyia wepesi njia ya kuiendea shari. Kama mnavojua wenyewe kujifunza elimu kunahitajia juhudi kubwa. Ndio maana akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kuchukua njia akitafuta kwayo elimu, basi Allaah atamfanyia wepesi njia ya kuelekea Peponi.”

Hii ni njia ndefu, ndefu ambayo hakuna waiwezayo isipokuwa wachache.

Wanatoka kila mwezi muda wa siku tatu. Kuendea nini? Hawajui. Kile wanachoambiwa ndio wanachosikiliza. Ni mamoja ni cha sawa au cha makosa. Hawajui kwa sababu kiongozi na raisi wao anayewaongoza yeye mwenyewe hajui.

Kutokana na haya unapasa kutambua kwamba, kama kunapatikana faida kadhaa katika baadhi ya Anaashiyd, hiyo hainaa maana kwamba ni kheri. Wanazuoni wanasema juu ya kila Bid´ah:

“Endapo ingelikuwa ni kheri basi Salaf wangetutangulia kuifanya.”

Haya ndio maneno yangu juu ya Anaashiyd za kidini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (158)
  • Imechapishwa: 05/07/2021