Tofauti kati ya kutahadharisha Ahl-ul-Bid´ah na kubadiy´

Swali: Kipindi hiki cha mwisho tunaona ´Awwaam, seuze wanafunzi, wanajiingiza katika masuala ya Tabdiy´ na Tafsiyq na kuwasema wanachuoni wakubwa wa Ahl-us-Sunnah?

Jibu: Jambo hili ni khatari. Sisi tunasema kuwa jambo hili hawajiingizi ndani yake isipokuwa na wanachuoni tu. Hata hivyo, kuna ambao wanasema kuwa mambo haya ni mapya. Tokea hili Ahl-us-Sunnah walisema hakuna yeyote anayefaa kuwaongelea wazushi isipokuwa wanachuoni tu? Kuna tofauti kati ya mzushi na Sunniy ambaye anatakiwa kufanyiwa Tabdiy´. Wazushi wanatahadharishwa hata na wasichana wa Ahl-us-Sunnah, ´Awwaam na wavulana. Wanasema kuwa huu ni Suufiy, Shiy´iy, Ikhwaaniy na kadhaa na kadhaa. Huyu ni mzushi katika Jamaa´t-ut-Jihaad, jumuiya ya al-Hikmah, Jamaa´at-ut-Tabliygh na kadhalika. Wazushi kama hawa wanaongelewa hata na ´Awwaam wa Ahl-us-Sunnah. Lakinji kuhusiana na Sunniy ambaye anatakiwa kufanyiwa Tabdiy´, huyu hakuna mwenye haki nalo zaidi ya wanachuoni tu. Ni kanuni na si mpya. Hatusemi kuwa haifai kuwaongelea kabisa wazushi isipokuwa wanachuoni. Hatusemi hivi. Hili linafanywa na wanachuoni na wasiokuwa wao. Lakini pale ambapo tunapotaka kumhukumu Sunniy ya kuwa ni mzushi, hakuna mwenye haki ya hili isipokuwa ni wanachuoni tu. Hili ni jambo liko wazi na kwa ajili hiyo utabainikiwa na mambo mengi.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Yahyaa al-Buraa´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=7035
  • Imechapishwa: 17/03/2018