Tofauti kati ya kufuru na shirki?


Swali: Kuna tofauti kati ya kufuru na shirki?

Jibu: Kufuru imeenea zaidi kuliko shirki. Kila mshirikina ni kafiri na sio kila kafiri ni mshirikina. Kafiri huyu anaweza kuwa mkanamungu na hatambui uwepo wa Mola kabisa. Kuhusu mshirikina anatambua uwepo wa Mola pamoja na kuwa anamshirikisha Yeye pamoja na wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (69) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/12-07-1438i.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2017