Swali: Baadhi ya wenye kutoa Khutbah wanazisoma Aayah za Qur-aan kwa utaratibu na wanaremba sauti wakati Khutbah inaendelea. Je, kitendo chao hichi kimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Kuna tofauti wakati mtu anapotoa Aayah kama ushahidi na wakati mtu anaposoma kama kisomo. Yule anayesoma kama kisomo anatakiwa kusoma kwa utaratibu na utungo. Yule anayesoma Aayah kama ushahidi hahitaji kufanya hivo kwa urataribu na utungo. Kwa sababu kitendo hichi kinachukua wakati wa watu na huenda wasizingatie ile maana ya Aayah. Wanachukulia kama kisomo tu. Usomaji wa Qur-aan imegawanyika aina mbili:

Ya kwanza: Kisomo kama kisomo. Hichi ndicho kinatakiwa kusoma kwa utaratibu na utungo.

Ya pili: Kisomo kama ushahidi. Hapa hapahitaji kusoma kwa utaratibu na utungo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
  • Imechapishwa: 20/10/2017