Tofauti kati ya istihaadhah na hedhi

Wanachuoni wanasema ya kwamba kuna tofauti tatu kati ya damu ya damu ya ugonjwa na hedhi:

1- Damu ya hedhi ni nyeusi tofauti na istihaadhah ambayo ni nyekundu.

2- Damu ya hedhi ni nene tofauti na istihaadhah ambayo ni nyembamba.

3- Damu ya hedhi inanuka tofauti na istihaadhah.

4- Madaktari wa leo wanasema kwamba damu ya hedhi haiwi imara. Inakuwa yaani bila kizuizi tofauti na istihaadhah ambayo inakuwa imara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath Dhiyl-Jalaal wal-Ikraam (1/406)
  • Imechapishwa: 24/09/2020