Tofauti kati ya Ibn Baaz na al-´Awdah kuhusu tofauti kati ya kundi lililookoka na pote lililonusuriwa

Swali: Je, ni kweli kuwa wewe unatofautisha kati ya kundi lililookoka na pote lililonusuriwa?

Jibu: Kundi lililookoka ndio pote lililonusuriwa. Ni wamoja.

Swali: Kwa hiyo hautofautishi kati ya hayo?

Jibu: Ni wamoja.

Swali: Jana jioni Salaam al-´Awdah[1] alikuwa na muhadhara na akasema kuwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz anaafikiana naye juu ya hilo.

Jibu: Hapana, hapana. Kundi lililookoka ndio pote lililonusuriwa na wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wao ndio Ahl-us-Sunnah, kundi lililookoka na wao ndio pote lililonusuriwa.

Swali: Na wao ndio Salafiyyuun?

Jibu: Na wao ndio Salafiyyuun. Wao ndio kundi lililookoka kwa kuwa wameokoka kutokamana na Moto, wameokoka kwa kuwa wameahidiwa kunusuriwa na wao ndio Ahl-us-Sunnah kwa kuwa wanafuata Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Salmaan al-´Awdah amesema:

”Kuhusiana na tofauti kati ya kundi lililookoka na pote lililonusuriwa, ni maoni waliotofautiana kwayo hapo kabla maimamu wakubwa akiwemo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Mwingine ambaye ameafikiana na mimi juu ya hilo ni Imaam, mlima na hoja, Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz (Hafidhwahu Allaah). Ameafikiana na mimi juu ya hilo. Amesoma kitabu na akafurahishwa na yaliyomo ndani yake. Nikamuomba aandike taaliki kukiwemo maoni yake juu ya hilo. Akaniahidi kuwa ataandika taaliki hiyo na kuieneza. Allaah (Ta´ala) amjaze kheri tele. Muhaddithuun wengine wengi katika nchi hii, Yemen, Misri na miji mingine ya Kiislamu wameafikiana na mimi. Hata kama maoni haya ni ya makosa lakini hata hivyo sio jambo kubwa… ” (https://www.youtube.com/watch?v=9jJcabonJGM&app=desktop)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=9jJcabonJGM&app=desktop
  • Imechapishwa: 19/11/2016