Mtasema kuwa Sufyaan bin ´Uyaynah amesema:

“Imani inashuka mpaka hakubaki katika imani chochote.”

Sufyaan hakika yuko pamoja na maimamu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Maisha yake yote amesema yale Ahl-us-Sunnah wanayosema. Katika moja ya vikao vyake alifafanua ´Aqiydah ya Salaf na kwamba imani inazidi na kupungua, ndugu yake akashangaa ambapo Sufyaan akakasirika na kusema:

“Imani inashuka mpaka hakubaki katika imani chochote.”

Enyi wajinga mlopewa mtihani! Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila sharti isiyokuwepo katika Kitabu cha Allaah ni batili hata kama itakuwa ni sharti mia.”

Hivyo mtasema kuna wanachuoni wengine wa Salaf walisema hali kadhalika. Hata hivyo haikuthibiti kwao. Hata kama imethibiti kwao hawakufanya kuwa ni istilahi waliyokuwa wakiitamka au kuwa ni sehemu yake au sharti ya maana ya imani. Hata na mimi naweza kusema hivo wakati fulani. Hata hivyo sifanyi tamko hilo kuwa ni sehemu wala sharti ya maana ya imani. Nilikuwa nikisema hivo kabla ya fitina za Haddaadiyyah. Lililo la ajabu kwa huyu Haddaadiy aliyepindukia Fawziy al-Bahrayniy ni kuwa anasema kwamba mimi nimesema katika moja ya darsa zangu kuhusu imani katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy:

“Imani ni maneno, matendo na I´tiqaad. Inazidi na kupungua mpaka hakubaki punje hata kidogo na inafikia mpaka kuwa chini kuliko hivo.”

Pamoja na hivyo ananituhumu Irjaa´. Kwa sababu kwa mujibu wake sikusema:

“Imani inashuka mpaka hakubaki katika imani chochote.” Tazama kitabu chake ”al-Qaasimah al-Khaafidhwah”, uk. 99.

Salaf wa mwanzo na waliokuja baada yao walikuwa wakisema:

“Imani ni maneno na vitendo. Inazidi na kupungua.”

Hawakutaja nyongeza hii. Ni wachache waliokuwa wakifanya hivo. Na wala hawakufanya kuwa ni sharti. Kwa mujibu wa Haddaadiyyah Salaf ni Murji-ah kwa kuwa hawakuweka hiyo nyongeza na wale wachache waliofanya hivo hawakuonelea kuwa ni sharti na wala hawakulitamka hovyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 09/10/2016