Hakika kisa cha ´Abdur-Rahmaan bin Muljim kina mazingatio makubwa. ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alimtuma Misri akafunze Qur-aan. Baada ya hapo akamuua ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh).

Pindi ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alipofikiwa na khabari ya kwamba Swabiygh anauliza maswali ya utata akamchapa mara mia moja. Baada ya kipigo cha kwanza akaletwa tena na kupigwa tena mara mia moja. Alipotaka kumpiga mara ya tatu Swabiygh akamwambia: “Ee kiongozi wa waumini! Ikiwa unataka kuniua basi niue.” Akamsafirisha kwenda Kuufah na akamkataza matangamano. Ikawa pale tu anapokuja kwenye mkusanyiko wa watu wanamkwepa. Baada ya muda akaja kwa kiongozi wa Kuufah na kumuapia ya kwamba vilivyokuwemo kichwani mwake sasa vimeondoka. Matokeo yake akamsitisia ususwaji[1].

Wewe, al-Halabiy, umeshikamana vipi na baadhi ya maneno ya Salaf:

“Mwenye kumtukuza mtu wa Bid´ah basi amesaidia kuubomoa Uislamu”?[2]

Hapa kunafuatia maswali yafuatayo ambayo nataka majibu yake:

1- Ni kwa nini kiongozi wa waislamu ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) alimpiga Swabiygh? Ni kwa nini alimwambia:

“Lau ningekuona una kipara basi ningekukata kichwa.”?

Hakusema hivyo kwa sababu alishakia kuwa ni katika Khawaarij? Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Alama yao ni kunyoa kipara.”[3]

2- Ni kwa nini alimsafirisha kwenda Kuufah? Ni kwa nini alikataza matangamano naye? Haikuwa kwa sababu ´Umar alichelea waislamu wasije kuathirika na fikira zake? Ndio.

Inapokuja kwetu – sisi wenye kusema kuwa tunafuata Hadiyt na mapokezi – inatustahikia kumkasirikia yule mwenye kusema mtu asichukui elimu kutoka kwa Khaarihiy au kutoka kwa yule mwenye kumtetea? Mtu kama huyu kweli anastahiki kupewa udhuru, kukaribishwa nyumbani, kusuhubiana naye na kutetewa? Hatakiwi kutolewa katika mfumo wa Salaf baada ya mtu kujua kuwa ni Khaarijiy?

Ninashangazwa na wewe, Shaykh ´Aliy, ambaye unajinasibisha na Ahl-ul-Hadiyth, kukaa kimya inapokuja katika kumtoa Khaarijiy katika Salafiyyah.

[1] Tazama Tafsiyr ya Ibn Kathiyr ”Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym” (07/413).

[2] Shu´b-ul-Iymaan (12/57) ya al-Bayhaqiy kupitia kwa Ibraahiym bin Maysarah.

[3] al-Bukhaariy (7562).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durar an-Najmiyyah fiy Radd-ish-Shubuhaat al-´Aqadiyyah wal-Manhajiyyah, uk. 382-385
  • Imechapishwa: 18/03/2017