Tofauti iliopo kwa wanachuoni kuhusu talaka tatu kwa wakati mmoja

Swali: Mwenye kusema: “Wewe umetalikika mara tatu”. Je, imepita?

Jibu: Hapa wametofautiana wanachuoni. Miongoni mwao kuko wanaosema kuwa imepita mara tatu kwa lafdhi moja, ingawa kufanya hivyo ni Haramu. Inapita pamoja na mtu kupata madhambi. Kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyoipitisha Talaka katika hedhi pamoja na madhambi. Talaka inapita pamoja na mtu kupata madhambi. Inakuwa ni Talaka ya Haramu lakini inapita. Haya ndio madhehebu ya wanachuoni wengi. Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah, Ibn al-Qayyim na kundi lingine la wanachuoni wanaona kuwa Talaka tatu kwa lafdhi moja inakuwa ni Talaka moja. Lakini rai hii haina ni nguvu. Bila kujali hata kama kuna wanachuoni waheshimiwa waliofutu rai hii, hata hivyo ni rai isiyokuwa na nguvu. Kwa kuwa aliokuwa akiihukumu ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhu) katika uongozi wake ni kuwa Talaka tatu zinapita kwa lafdhi moja. Naye ni Khaliyfah muongofu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/10070
  • Imechapishwa: 07/02/2018