Tofauti haihalalishi jambo la haramu


Swali: Kuna mwanaume mmoja ambaye mke wake alikuwa akifunika uso wake wakati anapotoka naye mbele za watu. Baada ya kuzungumziwa suala hili katika vyombo vya khabari wapo baadhi ya wanaume ambao wamedhoofika kwa kudhani kwao kwamba ni mambo yaliyo na tofauti na kwamba jambo lina wasaa ndani yake. Matokeo yake wake zao wakawa wanafunua nyuso zao kwa kuridhia waume zao. Ni zipi nasaha zako katika hilo?

Jibu: Tofauti haihalalishi jambo la haramu. Ikiwa kuna tofauti basi inayofuatwa ni dalili. Inatakiwa kuchukua maoni ya yule aliye na dalili na kumwacha yule asiyekuwa na dalili. Ama kusema kwamba masuala haya yana tofauti na kwamba jambo hili linaruhusu kwa sababu ni mambo yenye tofauti[1], basi itambulike kuwa tofauti haihalalishi jambo la haramu. Kuhalalisha na kuharamisha kunakuwa kwa mujibu wa dalili.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/kuna-tofauti-katika-mambo-haya-ima-mjinga-au-jitu-linalofuata-matamanio/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 25/09/2018